Proverbs 10:10-15


10 aYeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni,
naye mpumbavu apayukaye huangamia.


11 bKinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima,
lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.


12 cChuki huchochea faraka,
lakini upendo husitiri mabaya yote.


13 dHekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua,
lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu.


14 eWenye hekima huhifadhi maarifa,
bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi.


15 fMali ya tajiri ni mji wake wenye ngome,
bali ufukara ni maangamizi ya maskini.

Copyright information for SwhKC